Tuesday, April 9, 2013

KILINGE CHA GHANI,MITINDO NA MITAMBAO KUTOKA TAMADUNI MUSIC NDANI YA JIJI LA MBEYA, NI CLUB MARINA. KILA JUMAMOSI KUANZIA SA 8 MCHANA MPAKA 2 USIKU KIINGILIO 1000 TU WANAWAKE BUREEEEE. HIP HOP IS BACK MBEYA!!!!

Saturday, October 27, 2012

NEW JOINT IN TOWN FROM DI ACTION

NEW TRACK FROM DI ACTION FT FIDELOSSO,BEAT PRODUCED BY WILLY HD FROM M-LAB WHILE VOCAL&MIXING BY JAMVIBE RECORDS(PRODUCER BIZZO ONE) THE SONG BASED ON REAL LIFE OCOORED FROM SREET CHILDREN DUE TO LACK OF CARE FROM THE PARENTS 'DRUG USERS' SONG TILTLED SHULE YA MADAWA WRITTEN&COMPOSED BY DI ACTION FOR MORE ABOUT THIS SONG YOU CAN CALL 0764908211!

Tuesday, April 10, 2012

HII NI MAKALA ALIYOANDIKA MTANGAZAJI WA GENERATION FM KUHUSIANA NA JK KUTOA MIL.10 KTK MSIBA WA KANUMBA!

Yassin Wakwanza Juma
about an hour ago · .NAJUA WENGI WATACHUKULIA KIVINGINE LAKINI HUU KWA UPANDE WANGU NI UKWELI KABISA TENA UNAOUMIZA SANA..........
BORA NISEME NIWE NA AMANI

Makala haya, labda nayaandika huku tukiwa katika huzuni kubwa lakini kilichotokea hakiwezi kubadilishwa tena. Wengi watamzungumzia walivyomfahamu marehemu kwa kadri wanavyoweza, asilimia kubwa wakimsema kwa mazuri aidha kinafiki ama kutoka moyoni, wapo wanaolia kutokana na huzuni huku wengine wakiwa katika maigizo ya kawaida ya kutoa machozi. Hata wanafiki wapo wanajigalagaza na kujidai wanazimia ili waandishi waje kuwapiga picha. Na wengine wanazimia kutokana na mbanano lakini media zetu zitaandika mengine.
Asanteni wote ambao msiba umewagusa kwa namna ya kipekee. Na tujipe pole wale wote tuliojipeleka kimbelembele mapema pale Leaders club kama walivyotusisitiza kwenda kuaga halafu tukatemwa na kusahaulika umuhimu wetu kama mate yakishatoka mdomoni. Wameaga wanaojidai wana uchungu zaidi kuliko wote!!!! Hata kumwona mara ya mwisho tumeshindwa, nawachukia sana hawa jamaa waliojidai wao ndio waol na kuzima maamuzi ya familia

Ishu yangu leo ni kama ipo kisiasa lakini mimi hizo siasa sina huwa naweka wazi hisia zangu na mwisho wa siku natambua ujumbe unafika hata kama unamuumiza mtu!!!

Mkubwa wa nchi hii alikuwa mmoja kati ya watu wakubwa na kuheshimika kufika nyumbani kwa marehemu, jambo moja ambalo nililifurahia mwanzoni lakini leo hii nagundua sio jema ni kitendo cha jamaa kutoa shilingi milioni kumi kama rambirambi pale msibani kiukweli nimefikiria mengi sana, kwanza ni huu msiba, najua wajua kuwa huu sio msiba wa kitaifa japo umeligusa taifa. Sio kwamba nafurahia roho hii kutoweka, hapana marehemu alikuwa muhimu sana japo roho yake na ya babu yangu kijijini zote ni za kutoka na kurudi kule kule. “ROHO ZOTE NI SAWA USONI PA MUNGU!! ILA ZINATOFAUTISHWA NA UCHA MUNGU!! PEKEE”

Mkuu wa nchi ameonyesha udhaifu wa hali ya juu sana. Milioni kumi haikuwa pesa ndogo kama unavyoweza kuichukulia hasahasa katika kipindi hichi kigumu. Mkuu wetu wa nchi anaonekana bado ana ‘ujana’ ndani yake bado anatafuta kitu kinachoitwa sifa bila kutazama maslahi ya taifa letu.

Madaktari waligoma hapo majuzi, baba mama dada na kaka zangu walipoteza uhai kwa uzembe huu wa kushindwa kuwatimizia madaktari kile walichokuwa wamekitaka na baada ya vifo hivyo eti wakaongezewa malipio, sasa sijui serikali iliweka rehani roho za wapiga kura wake???
Halafu ulipanda ndege ukawa kama umeikimbia nchi, ukituacha katika vilio. Lakini nasikia hii ishu imesababisha ughaili safari ya kwenda huko sijui wapi kikazi. Yaani Baba wewe kwa kweli mi nasema baaaado!!!!

Ameugua mzee Kipara, nguli wa sanaa za maigizo hapa bongo, hakuna hata michango ya maana iliyoenda kuokoa roho yam zee huyu, akafariki!!!! Sikumbuki kama ulienda ama uliagiza mtu!!!!
Haya leo umetoa milioni kumi katika msiba ambao michango ya watu kadhaa ilikuwa inaweza kumzika katika kiwango hichi hichi alichozikwa JE AKIFA MSANII MWINGINE TENA UTATOA MILIONI KUMI AMA?? Siombei mabaya lakini jiulize itajengeka picha gani???. Baba siamini kama ulifikiria juu ya watoto wanaokaa chini huko kijijini kwetu, dawa za wagonjwa wa kifua kikuu zinaisha baba wanakufa tu mahospitalini na wengine majumbani huku.

Yaani binafsi ningekuona umefanya jambo la maana sana kama ungekuwa umewasaidia wasanii kabla hawajarejea mavumbini. Mtazame huyu bwana anayejiita STEPS……Hivi unajua kwamba marehemu na wasanii wengine hawachangii kabisa pato la taifa kwa sababu ya mambo ya kijanja janja yanayoendelea….anafaidika huyu STEPS. Sio mtanzania huyo baba, mimi sio mbaguzi wa rangi lakini haki za wasanii wetu ziko wapi sasa. Tazama hawana urithi wowote ule wafiwa, mtanzania usijidanganye na kazi nyingi za marehemu ukadhani ndo waliosalia wamepata utajiri, HAKUNA kazi zote zile alizofanya sio za kwake kashaiuza haki yake, kwa hawa WAHINDI!!!! Baba unaliona hili wewe, ama ndo vile kwa kuwa ni tukio la watu wengi tuone jinsi unavyowajali wasanii???? Huo ni unafiki baba!!!!!!

Watazame sasa wasanii, kama wakiwezeshwa hizo pesa ulizomwaga bila kujifikiria utawapatia waalimu kutoka vyuoni ambao serikali iliwapatia kilo saba za mchele na maharage kilo tatu eti wazitumie kwa mwezi mmoja. Baba kamati zako zina akili timamu na upendo kweli ama wanapuuzia watu wa hali ya chini na kujionyesha kwa wenye pesa??? Ndio hivyo unadhani tutafikiriaje sisi huku kijijini, babu na bibi kijijini wakisikia umefanya mambo kama haya unadhani watakuelewa baba….hebu sema mwenyewe MILIONI KUMI YA NINI?????? KWA NINI WASITOE PESA HAO STEPS WANAOTUIBIA KILA SIKU, Tena walitakiwa watoe kwa AMRI BABA!!!!! Yaani kama ungefanya hivyo ningekuona wa maana sana katika harakati za ukombozi!!!! Haiwezekani hata kidogo hawa jamaa wanachukua haki zetu kirahisi hivi, halafu tunabaki kugombana sisi kwa sisi Bongo Movies na TAFF!!!!!! Si umewasikia msibani sijui huyo muhindi anazungumzia HASARA atakayoipata baada ya Kanumba kuwa amefariki, huyu jamaa ni shetani MKUBWA aisee yaani unahojiwa unazungumzia hasara badala ya kuitazama ROHO!!!!!!!

Wao wanakula pesa wanaondoka. Haiwezekani eti mtu anatunga filamu anapewa milioni 20, naye anaridhika wakati hiyo milioni 20 ni sawa na watu 5000 kununua kazi hiyo, haya sasa watanzania tupo wangapi, tazama wajanja hawa wanavyotugandamiza baba!!! Tumekulilia mara ngapi wewe, mbona haujatujali, sasa hiyo pesa uliyotoa unadhani imeyaziba yale uliyojisahaulisha???? Pesa yako hiyo haijanufaisha chochote zaidi ya wajanja kadhaa waliokodolea macho pesa za rambirambi!!!!

Kwenye msiba wa mzee Kipara sijui walitoa laki ngapi vile,hawa jamaa eti kisa hajahusika katika filamu zao za STEPS kwa sana. Hawa sio wazuri baba??? Angalia nawewe unajichafulia jina lako zaidi aaah!!!!!

Sijamalizana na wewe baba, lakini kuna huu upande wa pili, hawa jamaa wa CHADEMA HAWA. Hivi hamjawahi kusikia kesi nyingine ama huyu LULU ndo kesi ya kwanza inayohusika na mauaji???? Mbona mwaleta siasa katika mambo yanayotuumiza kama haya. Kesi ya yule mtoto RAMA aliyekutwa na kichwa cha mtu mbona hamkusikika au kuna nini hapa kwa LULU??? RAMA yupo segerea sasa hivi mshawahi kuzungumzia hata hatma yake?? Sasa naduwaa eti mara Halima Mdee ameenda na cheti cha kuzaliwa mara sijui nini mbona RAMA alikuwa na miaka 16 wakati ule??? Binafsi nimekereka sana, halafu na huyu mama yake na Lulu, mbona wakati haka katoto kanafanya bethidei na kusema kametimiza miaka 18, mama alikaa kimya?? Halafu leo hii ananyanyua kinywa chake eti ‘mwanangu ana miaka 17” mimi simuhukumu lakini hizi siasa na zikome na sheria ichukue mkondo wake sasa!!!!! Kama she is innocent na iwe hivyo kama ni vinginevyo na hatua zichukuliwe.

Yaani siasa hizi zinakera na zinaonyesha ni jinsi gani tunakuwa na ubaguzi kwa walionacho na wasionacho. Mmeshindwa kuwatetea akina Babu seya na wanawe ambao hawajatoa roho za watu eti leo ghafla bin vuu LULU. Kwani yeye ni nani?????? Msitufanye sisi wajinga aiseee!!!! Mimi nasema haya najua wapo ambao hawawezi kusema, japo wanaumia mno!!!.

Waalimu wanalia kila siku maisha magumu, shule zina upungufu wa vifaa, miundombinu mibovu, maisha kwa ujumla yanapanda, nauli za daladala, bei za mchele na sukari. Halafu kweli baba unaenda kutoa milioni kumi wakati ulisema serikali haina pesa wakati unagoma kuwaongeza madaktari pesa hadi ndugu zetu wakafa hadi mochwari zikajaa maiti zikawa zinawekwa chini….ni nini kikuu katika hili mzee wetu??? Sikumsikia Obama kutoa mamilioni Michael Jacks alipotoweka, najua alituma mwakilishi kwenda kwenye mazishi lakini wewe baba unafanya mambo kama anayofanya mwernyekiti wa klabu ya Simba yaani yeye kila kitu, msemaji wa klabu yupo lakini kila jambo yeye hadi sasa amezoeleka. Mbona nawe unatufanya tukuzoee upesi hivyo.

Haya basi hata kama umetoa hiyo pesa ungefanya kimya kimya basi tusijue huku kijijini ambapo hospitali hazina madawa, ungefanya kwa siri baba wasisikie waalimu wanaoteseka kila siku, ungefanya kwa siri ili wale wazee wa TRL wasisikie maana uliwatesa sana, ungefanya kwa siri na watoto wa mitaani nao wasikusikie maana vilio vyao ni LAANA, ungefanya kwa siri basi zisikusikie zile nchi zinazotupa msaada maana Watadhani sisi matajiri baba, hivi kwa mfano wakikuuliza kwa nini umetoa milioni kumi utajibu nini???. Mkuu wangu sikutukani lakini ulichofanya UMEKURUPUKA na KUTAFUTA sifa zisizokuwa na maana.
MIMI NIMEMALIZA KINYONGO CHANGU!!!!! MOYONI SAAAAFI!!!!
LikeUnlike · ·Unfollow postFollow post · Share.
Elifazi Doctorfazi Mtwale and Grace Sambwe like this..

COMMENTS......

1.Hamis Mhando Daah! br. umenena, ila nnachokuomba makala hii iwekwe gazetin coz ktk fb inawafikia wachache wenye uwezo wa kutumia fb hao wengine watajuaje machungu haya?
Lingine, we unafikir baba alikusudia nin kutoa kiasi hicho jaji ktk mtazamo chanya ili sisi wazito kuelewa tupate kutafakar kwa pande zote kisha tufanye maamuz sahihi.15 minutes ago ·

JIANDAE KWA MECHI KALI KATI YA WATANGAZAJI MBEYA NA WATUMA SALAMU SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 14 KTK KIWANJA CHA SOKOINE

siku ya jumamoc itakua poa saana kwani ni mechi kali sana itapigwa pande za sokoine kati ya watangazaji na watuma salamu mchezo ambao mshindi ataibuka na zawdi ya mbuzi mkubwa mwenye thamani ya shilingi elfu 80 za kibofongo!!!!!!!!!!!!!!!! watangazaji kibao kutoka redio stations mbali mbali watahusika,MBEYA FM,SWEET FM,HIGHLANDS FM,ROCK FM,GENERATION FM,BARAKA FM,BOMBA FM NK.......... USIKOSE KIINGILIO BUREEEEEEEEEEEEEEEEE!!!

Friday, September 23, 2011

JCB MAKALA KUDONDOKA NA HARDMARD CHINI YA LAMAR.

toka pande za rap city chuga empire ya watengwa mtu mzima jcb makala anadondoka na bonge la ngoma akiwa na mtu mzima hardmard chini ya mkono wake lamar toka fishcrab mzigo ukiitwa dunia kizani.

SPEAK WITH YA BODY VIDEO KUONESHWA KWA MARA YA KWANZA LEO TRACE TV.

AY ft Romeo and Lamyia - "Speak with ya body" goes to air for the first time on Trace Urban today at 3pm

Tuesday, September 20, 2011

HAPPY B DAY DJ FREDY FROM 104.O BOMBA FM

HAPPY B DAY 2 YOU
HAPPY B DAY 2 YOU
HAPPY B DAY DEAR FREDY
HAPPY B DAY 2YOUUUUUUUUUU

WIMBO MAALUMU KWA AJILI YA DJ FREDY MOJA YA MA DJ WAKONGWE NDANI YA MKOA WA MBEYA. MUCH RESPECT KWAKO PIA

Friday, September 16, 2011

MBUNGE WA MBEYA MJINI MH JOSEPH MBILINYI AKA SUGU ATEMBELEA SOKO LILILOUNGUA NA KUWAPA POLE WALIOPOTEZA MALI ZAO!!!

MA HOME BOY BROTHER.


MZIGO MKUBWA IZINEEEEE AAIR ,KUTOKA KUSHOTO ,D.ACTION ,MCHIZI KICHIZI ,INCREDIBLE PRESENTER GOD FATHER MPANGO MZIMA,JAMAA WASOME KUPITIA 90.7 SWEET FM MBEYA MZIGO MKUBWA ANGANI.

Saturday, September 10, 2011

SWEET FM MBEYA YAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KATIKA MAOMBOLEZO YA MSIBA WA TAIFA.

SWEET FM MBEYA PIA YATOA POLE KWA WALE WOTE WALIOFIKWA NA MSIBA HUO BAADA YA AJALI YA MELI KATIKA BAHARI YA HINDI NA KUPOTEZA WATANZANIA WENZETU ZAIDI YA 200!

SALHA ISRAEL ALAMBA MKOKO WA VODACOM JANA NIGHT!

bidada salha israel aibuka mshindi wa shindano la miss tanzania 2011 hapo jana usiku.watu kibao walikuwa happy baada ya salha kutangazwa mshindi kutokana na kuwashika raia na swaga zake.

MH! HILI TABASAMU ALIJUA YEYE NI MSHINDI NI NN? teh teh teh

AKILI THE BRAIN APANDA JUKWAANI

MKALI AKILI THE BRAIN USIKU HUU AMEPANDA JUKWAANI KATIKA SHINDANO LA KUMTAFUTA MISS TZEE MSHIKAJI KALUDI POA NA MTOTO MMOJA WA KIDOSHO ILIKUWA POA SANA

USAILI WA BLACK TALLENT UMEANZA LEO.

katika ukumbi wa miami usaili wa mashindano ya kuimba,kucheza na ku free style umeanza leo hii na much respect wote waliokuwepo pande zile pamoja na producers,q.base kutoka tabasamu rec,zesti kutoka moja moja rec, na wana kibao toka pande za ice angl

e.

MNYALU AKANUSHA KUHUSIANA KUWA NA STUDIO MBEYA!

ishu iliyokuwepo kitaa kuhusiana na baadhi ya wasanii kudai wamerekodi ngoma zao katika studio ya mike t iliyopo jijini mbeya imegundulika kuwa si kweli kwani mike t alipotupiwa swali kama anamiliki studio ndani ya mbeya alikanusha vikali na kudai ana studio morogoro iitwayo myke rec na dizinga ni show biz defined inayo deal na vedeo na sio mbeya. so sio issue kwa washkaji wanao inuka katika redio stations mbalimbali jijini mbeya na kudai wamefanya track katika studio ya mnyalu iliyopo mbeya......

mnyalu!

Friday, September 9, 2011

ALBUM YA MZAZ LIL WAYNE YAONGOZA KWA MAUZO TANGU IDONDOKE SOKONI!!!!!!!!

HAPPY B DAY PROD,LOSSO!


LOSSO FROM MASHADA INC PRODUCTION!

MSAMIATI

SWALI LA KIZUSHI KWA MSAMIATI LILIKUWA NI KWA NINI KITAMBO YUPO KIMYA KATIKA GAME NA JIBU ALILOTOA NI KWAMBA MAMBO YA SKULI NDIO DIZAINI YANABANA BUT SOON ATARUDI FULL KATIKA GAME. MUCH RESPECT KWAKE MCHIZI ANAYEWAKILISHA PANDE ZA T.BLOCK IN DA GREEN CITY!

ay ft romeo